Meli kubwa ya mizigo yenye urefu wa mita 150 kutoka nchini Urusi, imewasili na kutia nanga kwenye bandari ya Tanga, baada ya kukamilika kwa ujenzi wa gati lenye urefu wa mita 300.
Meneja wa Bandari Tanga, Masoud Mrisha amesema Meli hiyo imebeba shehena ya mbolea kwa ajili ya viwanda vya madini, na ujio wake ni matunda ya uwekezaji uliofanywa na Serikali.
Amesema Meli hiyo imebeba mzigo wa tani 6909, unaopelekwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo – DRC na utaanza kushushwa hii leo Februari 27 -28, 2023.