Mtangazaji maarufu wa kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM, Millard Ayo amepiga hatua nyingine kwa kuongeza wigo wa kazi yake kuzihesabu habari muhimu za siku, akipewa ‘mchongo’ mwingine na kituo cha Televisheni cha Kenya ‘Citizen TV’.

Mtangazaji huyo ameweka wazi mchongo wake mpya wa kuripoti habari za burudani kutoka Tanzania kwenye kituo hicho kikubwa nchini Kenya.

“Kuanzia January hii mtu wako wa nguvu Millard Ayo nimeanza kuonekana CITIZEN TV Kenya nikiripoti habari za Entertainment kutoka Tanzania,” alitweet.

Hata hivyo, kwa mashabiki wa Millard kupitia Amplifaya hawapaswi kutikisika na habari hii kwani ataendelea kupiga kazi ya Clouds FM kama kawaida, kilichoongezeka ni ‘mchongo’ mwingine wa kuingiza kipate cha nguvu.

Millard alikuwa mtangazaji wa kwanza nchini kuwa na ‘maripota’ wa habari mbalimbali nchini na katika nchi nyingine Afrika Mashariki. Mfumo huo aliouanzisha umemgekia yeye na kumpa chanzo kingine cha kipato.

 

Rooney afunguka ya moyoni baada ya kuifikia rekodi ya magoli ya Charlton
Diamond kufunika ufunguzi wa Kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2017’