Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan yupo nchini Ethiopia kuhudhuria mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU).

Rais Samia mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa leo Februari 16, 2023, alikaribishwa na kukagua gwaride la heshima.

Rais Samia anahudhuria mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU).

Aidha, mama pia alipata fursa ya kuangalia ngoma za asili za Taifa la Ethiopia kwenye uwanja huo wa ndege wa Kimataifa wa Bole kabla ya kwenda sehemu aliyoandaliwa kupumzika.

Jana, Februari 15, 2023 Rais Dkt. Samia aliwaapisha Viongozi wateule katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawariri na Makatibu wakuu.

Mauaji na ukatili: Polisi yaja kivingine
Familia ya marehemu 'AKA' yatoa taarifa hii mpya