Mmiliki wa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Moise Katumbi amehukimiwa kifungo cha miaka mitatu jela.

Mfanyabiashara huyo tajiri, amekumbwa na adhabu hiyo yeye mwenyewe akiwa nje ya nchi kwa matibabu.

Bilionea huyo mwenye umri wa miaka 51 amekutwa na hatia ya kujimilikisha na kuuza jengo kinyume cha sheria mjini Lubumbashi, ambako ni ngome yake kuu ya kisiasa.

Na hayo yanatokea wakati tayari amependekezwa na vyama vya sita vya siasa kugombea Urais wa DRC unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu.

Rais Joseph Kabila, ambaye yuko madarakani tangu mwaka 2001, anakaribia kumaliza kipindi chake cha pili cha utawala na kwa mujibu wa Katiba anatakiwa kustaafu Desemba.

Lakini kuna hisia kwamba hukumu hiyo ni shinikizo za kisiasa ili kumvunja nguvu Katumbi, ambaye anapewa nafasi kubwa ya kuwa Rais mpya wa DRC.

Mahakama ya Lubumbashi, mji wa pili kwa ukubwa DRC, pia imempiga faini ya dola za KImarekani Milioni 4.1 kwa kosa la kuuza jengo hilo ambalo raia huyo wa Ugiriki amesema ni mali ya famili yake.

Katumbi alisafiri nje ya nchi Mei 20, mwaka huu wakati tayari imekwishatolewa hatu ya kukamatwa kwake.

Katumbi anatarajiwa kukatia rufaa hukumu hiyo.

Wabunge Marekani wakaa ‘sakafuni’ kususia Bunge, wadai sheria kali umiliki silaha
Ziara ya Maalim Seif Pemba yazua Jambo, Polisi walaani