Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Zimbabwe (MDC) na mpinzani mkuu wa Rais Robert Mugabe, Morgan Tsvangirai, amepelekwa Afrika Kusini kwaajiri ya matibabu.

Wafuasi wa chama chake wamesema kuwa hali yake sio mbaya lakini wameamua kumpeleka Afrika Kusini kutibiwa katika hali ya utulivu kwani amekuwa akifanya kazi kwa muda mrefu bila kupumzika.

Aidha, mwaka jana Tsvangirai alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa saratani hivyo kutakiwa kuhudhuria mara kwa mara hospitalini kwaajiri ya kupatiwa matibabu ya karibu zaidi.

Hata hivyo, watu wengi nchini Zimbabwe wanahoji iwapo kiongozi huyo wa upinzani nchini humo kama ni mzima wa afya baada ya afya yake kuonekana dhaifu.

 

Magazeti ya Tanzania leo Septemba 17, 2017
Nyumba ya Zitto Kabwe yateketea kwa moto