Mshambuliaji kutoka nchini Zambia na Klabu ya Simba SC Moses Phiri amechimba Mkwara kuelekea mchezo wa Mzunguuko wanne wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Hatua ya Makundi dhidi ya Vipers SC ya Uganda.

Simba SC itakuwa mwenyeji wa mchezo huo wa Kundi C, kesho Jumanne (Machi 07), katika Uwanja Benjamin Mkapa, huku ikihitaji ushindi ili kujihakikishia njia ya kutinga hatua ya Robo Fainali.

Phili amesema wamejiandaa vizuri kuikabili Vipers SC, na wanatambua umuhimu wa mchezo huo ambao, unasubiriwa kwa hamu kubwa na Mashabiki wa Soka nchini Tanzania na Uganda.

“Tumepata alama tatu za mchezo wa ugenini, ulikuwa mchezo mgumu kwetu kutokana na mazingira ya kucheza ugenini, lakini jambo kubwa ni kuwa tulifanikiwa kupata ushindi wa kwanza na alama tatu muhimu.”

“Mchezo wa Jumanne ni muhimu kwetu kwani ni kama rasmi tumeanza safari yetu ya kufuzu hatua ya Robo Fainali, tunahitaji ushindi na tutapambana kushinda mchezo huu na iliyosalia ili kuhakikisha tunatimiza malengo yetu kama timu ya kucheza nusu fainali ya mashindano haya.” amesema Phiri

Mepema leo Jumatatu (Machi 06) Kikosi cha Vipers SC kiliwasili jijini Dar es salaam, tayari kwa mchezo dhidi ya Simba SC ambayo imekuwa kwenye maandalizi tangu Ijumaa (Machi 03), baada ya kumaliza mchezo wa 16 Bora Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ dhidi ya African Sports ya Tanga iliyokubali kufungwa 4-0, Uwanja wa Uhuru.

Tanzania Prisons yaivizia Namungo FC
Waandishi, Wachambuzi waaswa sakata la Fei Toto