Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, ameitaka Klabu ya Real Madrid kuachana na mpango wa kutaka kusajili mlinda lango namba moja wa timu hiyo, David De Gea.

Real Madrid imekuwa ikihusishwa na kumtaka golikipa huyo kwa udi na uvumba kutokana na kiwango bora alicho nacho kwa wakati huu, mwaka 2015, De Gea alikaribia kujiunga na miamba hiyo ya Hispania kuchua nafasi ya Golikipa aliopo hivi sasa, Keylor Naves lakini dili hiyo haikufanikiwa.

Akiongea na wanahabari, Jose Mourinho amesema itabidi Real Madrid kutazama sehemu nyingine na kusisitiza kuwa De Gea hawezi kwenda popote.

“Ataendelea kukaa hapa. Sijui maazimio ya Real Madrid lakini ningekuwa wao, ningetazama kwingine,” amesema Mourinho.

Madrid, ilikuwa karibu kumpata mlinda lango wa Athletic Bilbao Kepa Arrizabalaga mwezi Januari, na pia inahusishwa na kumtaka mlinda lango wa Chelsea Thibaut Courtois.

Nsato: Matukio ya uhalifu nchini yamepungua, jeshi liko imara
Rapa Rick Ross Kutumbuiza Nchini Kenya