Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amewataka maafisa habari za wizara zote kuimarisha mahusiano na waandishi wa habari ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Ametoa maelekezo hayo alipokutana na na wakuu wa vitengo vya mawasiliano serikalini kutoka wizara zote Jijini Dodoma ambapo lengo ni kujadilimaswala mbalimbali ikiwemo kuboresha vitengo hivyo katika utoaji wa Taarifa za Serikalini.

“Tafuteni namna nzuri za kushirikiana na vyombo vya habari, mkiimarisha mahusiano mazuri na waandishi wa habari, mtafanya kazi zenu kwa urahisi,” amesema Msigwa.

Naye Mkurugenzi Msaidizi (Mawasiliano Serikalini), Zamaradi Kawawa amewataka maafisa hao kuimarisha mahusiano na wadau wao wote.

“Tuwe na mahusiano mazuri miongoni mwetu, pia baina yetu na watumishi wenzetu wa wizara zetu na wizara nyingine.”

Itakumbukwa mwaka 2005 Serikali ilianzisha vitengo vya mawasiliano serikalini na mwaka 2016 serikali ikapitisha Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa ili wanahabari na wananchi wapate taarifa za utendaji kazi wa Serikali kwa urahisi.

Watumishi wa afya wasimamishwa kazi JNIA kwa utoro kazini
Chanjo ifike na vijijini - Naibu Waziri