Msumbuji imeiambia jamii ya kimataifa aina ya msaada inaohitaji kukabiliana na uasi unaohusishwa na kundi linalojiita Dola la Kiislamu – IS, lakini kwa sababu za uhuru wa nchi itayashughulikia mambo kadhaa ya tatizo hilo bila kusaidiwa.

Rais wa Msumbuji, Filipe Nyusi ameyasema hayo wiki mbili baada ya shambulizi la wanamgambo wa itikadi kali katika mji wa pwani wa Palma, karibu na miradi ya gesi asilia ya thamani ya mabilioni ya dola ambazo zinapaswa kuuimarisha uchumi wa nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika.

Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC inafanya mikutano jana na leo kuzingatia jibu la kikanda kwa uasi huo, wakati Marekani tayari ina timu ndogo ya Vikosi Maalum vya Kijeshi nchini Msumbiji katika ujumbe wa mafunzo.

Sanga: Simba SC bingwa 2020/21
Semunyu: Tshibangu amedanganya, aseme ukweli