Serikali kupitia Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, imewataka wananchi kuwekeza katika viwanda vidogo vidogo vya kuzalisha bidhaa mbalimbali ili kukuza vipato.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alipotembelea maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi yanayoendelea Mjini Dodoma.

Amesema kuwa hali ya Watanzania kuanzisha viwanda vidogo vidogo itasaidia kuongeza kipato chao na kuweza kuinua Uchumi wa Taifa.

“Maonyesho haya yanalenga kuwaonyesha Watanzania kuwa Serikali kupitia taasisi zake inatoa huduma muhimu za kuendeleza Sekta ya Viwanda vidogo vidogo, hii itajenga uchumi wa mtu mmoja mmoja na wa taifa na itaongeza ajira,”amesema Mwijage.

Kwa upande wake, Meneja wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Tatu Mwaruka amesema kuwa taasisi hiyo husaidia mikopo na kusaidia kuanzisha miradi mbalimbali kwa jamii.

Maonyesho hayo yanayoendelea Mkoani Dodoma yameandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa lengo la kutoa somo kwa wananchi kuhusu uwekezaji wa viwanda vidogo vidogo.

Video: Jokate aivuruga UVCCM, Mgogoro CUF wazidi kuwaka moto
Magazeti ya Tanzania leo Aprili 24, 2017