Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye, amesema kuwa ni makosa makubwa kuwahukumu moja kwa moja watuhumiwa wa madawa ya kulevya kuwa wanajihusisha na biashara hiyo.

Amesema kuwa licha ya kuunga mkono juhudi za kupambana na biashara na matumizi ya dawa za kulevya, amesema busara inapaswa kutumika katika kuwabainisha watuhumiwa kwa sababu bado hawajahukumiwa na mahakama.

“Ni muhimu kulinda haki ya mtuhumiwa, jambo lenye mjadala ni busara inayotumika kushughulika na wahusika ili kusaidia vyombo vingine na wanaosambaza kuweza kupatikana,tusiwahukumu kwa tuhuma hasa wasanii maana kujenga brand ni kazi kubwa,”amesema Nape.

Aidha, tangu kuibuka kwa sakata hilo,wadau mbali mbali wamekua wakikosoa utaratibu huo kwa kueleza kuwa wasanii kuhukumiwa kabla ya uchunguzi kubainika kama wanajihusisha na biashara hiyo siyo mzuri.

Wasanii wanaochunguzwa kwa tuhuma hizo ni Khalid Mohamed (TID), Dogo Hamidu, Wema Sepetu na Babuu wa Kitaa, wengine ambao wametakiwa kufika katika kituo kikuu cha polisi kuhojiwa ni Vanessa Mdee na Tunda Sabasita.

Hata hivyo Nape amesema kuwa wapo watu wa kada mbali mbali wanaotumia dawa za kulevya, lakini wasanii wanaonekana zaidi kwa kuwa ni maarufu na kubainisha jinsi serikali kupitia Wizara yake inavyowasaidia kuonokana na matumizi ya dawa za kulevya.

Lipumba: Naumia sana kukwazana na Maalim Seif
Video: Familia ya Wema, Diamond wapiga kambi Polisi Dar, Lipumba: Ukawa ilitaka kuizika CUF