Tume ya Taifa ya Uchaguzi Nchini – NEC, imeanza maandalizi mbalimbali ikiwemo kufanya jaribio la uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura kwa Mkoa wa Tabora na Mara kwa majaribio.
Hatua hiyo, itawezesha wapiga kura ambao wameandikishwa na wapo kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura kuanza mchakato wa kubadili na kuboresha taarifa zao na kituo cha kupiga kura iwapo amehama Mkoa au Wilaya nyingine kurekebisha taarifa kwa kutumia simu ya mkononi.
Hii inamaanisha kuwa, utaratibu huo hautohusu wapiga kura wapya au wale waliopoteza kadi ama ambao kadi zao zimeharibika ambapo vyama vya siasa nchini pia vitashiriki kwa kuweka Wakala kwa kila kituo ha kuandikisha wapiga kura ili kujiridhisha na hatua zinazochukuliwa.
Zoezi hilo, pia linahusisha kupima uwezo wa vifaa na mifumo ya uandikishwaji itakayotumika wakati wa uboreshaji wa datfari la kudumu la wapiga kura na kwa mujibu wa wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa NEC, Kailima Ramadhani amesema watatumia BVR kits zenye vifaa vinavyowasiliana, ili kuchukua na kutunza taarifa za wapiga kura.
Amesema, “uboreshaji huo utahusisha kuandiskisha raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka18 au zaidi na atakayetimiza umri wa miaka 18 kabla au ifikapo tarehe ya uchaguzi wa mwaka 2025. Tume imesanifu na kuboresha mfumo wa uandikishaji wa kupiga kura(Votes Registration system -VRS ili kukidhi muundo wa BVR kits za sasa.”
Vifaa hivyo ni tofauti na vile vilivyotumika mwaka 2015 na 2019, ambavyo zilikuwa zinatumia program ya Microsoft Windows tofauti na vya sasa ambavyo vinatumia program ya Android mchakato wa kufanya uchaguzi mdogo wa Serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka ujao, kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.