Shirika la Bima la Taifa (NIC), limetoa elimu kwa mawakala na wadau kuhusu huduma za Kidijitali ili kuendana na Kasi ya maendeleo ya kibiashara.
Akizungunza wakati wa semina hiyo, kaimu Mkurugenzi shirika la bima la Taifa (NIC), Harobert Polepole amesema elimu imetolewa Kwa watumishi wa umma na wadau ili kuboresha mahusiano ya jamii na kutambua faida za bima.
Amesema shirika hilo kwasasa lina uwezo kuhudumia wateja ndani ya siku saba na kulipwa stahiki zao kwa wakati na kuongeza kuwa, “tunaendelea kutoa elimu Kwa wananchi wajiunge na Boma zetu ili ziweze kuwanifaisha pindi yanapotokea majanga au chamgamoto yoyoye.”
Aidha, amesema elimu hiyo ya kidigitali imesaidia Katika utoaji wa huduma na kuongeza wateja ambapo kila mwezi zaidi ya wateja wapya 500 hujiunga na huduma za bima huku baadhi ya mawakala akiwemo Estomi Malay kutoka Kilimanjaro akisema, mfumo huo utarahisisha utendaji kazi na kua na manufaa Zaidi
Hata hivyo, ameongeza kuwa mfumo huo utasaidia hata wateja waliopo mbali ambapo watatumia teknolojia katika kuwahidumia tofauti na awali walilazimika kutumia muda mrefu kufikisha huduma.