Kiungo wa mpira mtoto wa Gisenyi Rwanda, Haruna Niyonzima ataagwa rasmi na klabu yake ya Yanga kwenye mtanange wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Ihefu SC, dimbani Benjamin Mkapa Alhamisi ya Julai 15, 2021.

Kiungo huyo alitua nchini na kuanza kuitumikia Yanga kwenye msimu wa mwaka 2011/2012 na kufanikiwa kutwaa mataji manne ya Ligi Kuu akiwa na Yanga SC na mawili akiwa na Simba SC.

Wenyewe Yanga wamepanga kuutumia mtanange wao wa Alhamisi ya Julai 15, kumuaga Mnyarwanda huyo huku Ihefu nao wakiutamani mchezo huo kwaajili ya kujitetea na lindi la kushuka daraja.

Kwa sasa Ihefu ina alama 35 kwenye msimamo wa ligi ikiwa nafasi ya 15, huku waliopo chini yake ni Gwambina FC na Coastal Union wenye pointi 34 kila timu.

Ihefu inazihitaji alama tatu kutoka kwa Yanga SC hapo Alhamisi ili kuzivuta shati Mbeya City na JKT Tanzania wenye pointi 36 kila moja.

Yanga nao wanahitaji kushinda mtanange huo ili kumuaga vema kiungo wao huyo aliyerejea klabuni hapo Januari, 2020 nyakati za dirisha dogo na mechi yake ya kwanza ilikuwa ni dhidi ya Simba Januari 4, 2020, iliyomalizika kwa sare ya 2-2.

Wanaouza 'ARDHI' wapewa onyo
Watumishi wa afya wasimamishwa kazi JNIA kwa utoro kazini