Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ametoa onyo kwa wenyeviti wa vijiji wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro wanaojihusisha na kuuza ardhi ya vijiji bila kufuata taratibu.
 
Ametoa kauli hiyo alipozungumza na wananchi wa kata ya Dumila wilayani Kilosa mkoani hapo akiwa katika ziara yake ya kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi kero za ardhi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara katika Mkoa huo na kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusiana na migogoro ya ardhi.

Dkt. Mabula amesema, migogoro mingi ya ardhi imekuwa ikisababishwa na wenyeviti wa vijiji hasa katika suala zima la ugawaji ardhi na kusisitiza kuwa, jukumu la kugawa ardhi ya kijiji kwa mujibu wa sheria ni mkutano wa kijiji na siyo mwenyekiti.
 
 ‘’Naomba muelewe kuwa mwenyekiti wa kijiji haruhusiwi kugawa ardhi na yeyote atakayepewa ardhi na mwenyekiti wa kijiji basi ajue imekula kwake’’ amesema Dkt Mabula.
 
Aidha amemuagiza Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Morogoro Frank Minzikuntwe kuwapitisha katika sheria ya ardhi ya usimamizi viijiji wenyeviti wa vijiji ili waweze kuielewa na kusimamia vizuri ardhi katika maeneo yao.

Rais Mwinyi akabidhiwa ripoti uchaguzi Mkuu zanzibar
Niyonzima kuagwa kwa heshima Young Africans