Rais wa Shirikisho la soka la Ufaransa ‘FFF’ amesimamishwa kazi kwa kosa la kutoa kauli iliyomkosea heshima Mkongwe wa soka Zinedine Zidane.

Noel Le Graet (81) amekuwa akishambuliwa vikali tangu wikiendi iliyopita baada ya kusema, “Sitopokea simu ya Zidane kama atanipigia kuhusu kuiongoza timu ya taifa ya Ufaransa”.

Le Graet alianza kwa kuulizwa kuwa atafanya nini ikiwa Zidane atapewa kazi Brazil, naye alijibu “sijali, anaweza kwenda popote anapotaka, yeye hufanya anachokitaka, hainihusu, sijawahi kukutana naye, na sisi hatujawahi kufikiria kuacha kufanya kazi na Didier Deschamps”

“Anaweza kwenda popote anapotaka, kwenye klabu….. kama akijaribu kunipigia, sitopokea hata hiyo simu yake”.

Maneno hayo yamekosolewa vikali na mashabiki wa soka nchini humo huku baadhi ya watu mashuhuri kama nyota wa PSG Kylian Mbappe na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wakionyesha kutokubaliana na kauli hiyo.

Zidane huchukuliwa kama shujaa nchini humo baada ya kombe la Dunia la mwaka 1998 ambapo Ufaransa ilishinda kwa kuifunga Brazil 3-0.

Katika mechi hiyo mkongwe huyo alifunga mabao mawili na alikuwa mchezaji bora wa mechi.

Rage amshauri tena Feisal Salum
Jean Baleke: Ninasubiri ruhusa TP Mazembe