Mbunge wa zamani wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye ametangaza kukihama Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kuhamia UDP.

Goodluck Ole Medeye (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo katika makao makuu ya chama hicho

Goodluck Ole Medeye (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo katika makao makuu ya chama hicho

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika ofisi za chama chake hicho kipya, Medeye ameeleza kuwa ameamua kusimamia demokrasia na kwamba amekerwa na mwenendo wa Chadema dhidi ya Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson.

Medeye aliondoka CCM na kuhamia Chadema katika vuguvugu la Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana.

Video: Wabunge wa Ukawa wataka Posho za vikao vya Bunge zifutwe
Chadema Waifikisha Serikali Mahakama kuu