Klabu ya Liverpool inafikiria mpango wa kuvamia Wolverhampton Wanderers kwenda kunasa huduma ya winga Pedro Neto kwa ajili ya kumtumia msimu ujao.

Katika uhamisho wa dirisha lililopita la majira ya kiangazi, kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp alikuwa bize kufanya usajili wa wachezaji wa kiungo baada ya kupoteza wakali kadhaa kwenye eneo hilo.

Lakini, katika kuelekea dirisha la majira ya kiangazi la mwakani, Liverpool inajiandaa mapema kwa kuhitaji saini ya staa wa Wolves, Neto ili kutokuwa kwenye wasiwasi mashaka makubwa endapo kama Mohamed Salah ataondoka kutokana na mchezaji huyo kupigiwa hesabu na Saudi Pro League.

Liverpool iligomea ofa ya Pauni l50 Milioni ya kumuuza Salah kwenda huko Mashariki ya Kati kwenye dirisha lililopita.

Tangu msimu huu uanze, Neto amekuwa kwenye kiwango bora san akirejea uwanjani baada ya kuwa nje kwa miaka miwili kutokana na kuwa majeruhi.

Msimu huu, Neto amefunga bao moja na kuasisti mara nne katika mechi saba.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Oktoba 5, 2023
Julio, Pawasa waanika udhaifu Simba SC