Picha ya kusikitisha inayomuonesha mjamzito akijaribu kutoroka kupitia dirisha la juu akiomba msaada baada ya magaidi wa IS kushambulia eneo alilokuwepo jijini Paris Ufaransa imeendelea kuwa maarufu ikigusa hisia za watu wengi.

Mwanamke huyo aliyekuwa mmoja kati ya mamia ya watu waliokuwa kwenye ukumbi wa Bataclan alionekana akining’inia kwenye dirisha moja huku akipiga kelele za kuomba msaada na kueleza kuwa yeye ni mjamzito.

“Help, help I’m pregnant, I’m pregnant. What shall I do..?” alisikika mwanamke huyo kwa sauti ya juu iliyojaa hofu wakati magaidi wakiendelea kufyatua risasi katika maeneo mengine.

ukumbi wa Bataclan baada ya shambulizi la kigaidi Ijumaa Usiku

ukumbi wa Bataclan baada ya shambulizi la kigaidi Ijumaa Usiku

Kwa bahati nzuri, taarifa zinaeleza kuwa mama huyo mtarajiwa aliokolewa na wasamalia na anasadikika kuwa alisalimika.

Katika hatua nyingine, mwanamke wa Kimarekani, Hellen Wilson ambaye alinusurika katika shambulizi hilo alieleza kuwa magaidi hao walikuwa wakimimina risasi bila kujali na kwamba waliwashambulia walemavu waliokuwa kwenye ‘wheelchairs’.

Samwel Sitta, Dkt. Nchimbi wakatwa Rasmi Uspika, Hawa ndio wamepitishwa
Wastara Atoa ya Moyoni Kuhusu Kukatwa Mguu Wake