Washukiwa tisa wa ujambazi ambao walikuwa wakijihami kwa silaha, wameuawa na Polisi wakati wa majibizano ya risasi nchini Afrika Kusini.

Waziri wa Polisi nchini humo, Bheki Cele amesema katika mashambulizi hayo, washukiwa wengine watatu walijeruhiwa eneo la tukio katika kitongoji cha Sebokeng kilichopo kusini mwa jiji la Johannesburg na kwamba hali zao ni mbaya.

Amesema, washukiwa hao, waliaminika kuhusika na wizi wa silaha kwenye magari ya kubebea pesa katika eneo hilo na walikuwa karibu kuanzisha wizi mwingine na walidhibitiwa baada ya habari zao kusambaa.

Katika eneo hilo, pia Silaha sita na vilipuzi vilipatikana katika eneo la tukio na Cele alisema kulikuwa na magari matatu nje ya nyumba wakati polisi walipofika mahala hapo majira ya asubuhi na upelelezi juu ya tukio hilo bado unaendelea ili kubaini mtandao wa kundi hilo.

Kocha Hans amkataa Mkude Singida Big Stars
Serikali yafikiria kuharamisha ajira za kigeni sekta ya Afya