Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tff imekiruhusu chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA kuendelea na mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa chama cha soka wilaya ya Temeke (TEFA) kama ulivyopangwa na kamati ya uchaguzi ya  chama hicho.
Baada ya ruhusa hiyo Uongozi wa DRFA umemuandikia barua katibu wa TEFA Kasim Mustapha ili aijulishe kamati ya uchaguzi ya chama hicho kuendelea na mchakato huo kama kawaida.
Awali TFF iliiandikia barua DRFA kushauri kusimamishwa kwa uchaguzi huo,kutokana na kile kinachoonekana kuwepo na malalamiko kuhusu mchakato wake lakini maada ya mashauriano kati ya pande hizo mbili,sasa ni ruksa kwa uchaguzi huo kufanyika kesho jumapili Agosti 16,2015 kama ulivyopangwa.
Aidha DRFA imewaomba wapiga kura wote kujitokeza kwenye uchaguzi,huku ikisisitiza amani na utulivu itawale katika zoezi hilo muhimu la kuwapata viongozi watakaokiongoza chama cha soka Temeke,ili kuleta maendeleo ya mpira wa miguu mkoa wa Dar es salaam.
 
IMETOLEWA NA DRFA

MALINZI AMPONGEZA NDIKURIYO
Ukawa: Amri Ya Polisi Kuzuia Maandamano Haituhusu