Uamuzi wa jeshi la Uturuki kuiangusha ndege ya kivita ya Urusi katika mpaka wake na Syria Jumanne wiki hii umezua taharuki kubwa huku mataifa hayo mawili yakitoa matamko tofauti yenye mlengo wa tambo.

ngege ya Urusi

Uturuki ilisema kuwa iliamua kuidungua ndege hiyo kwa kuwa ilikiuka taratibu za Anga za Uturuki na kwamba ilipuuzia tahadhari 10 zilizotolewa na Jeshi hilo.

“Ndege ya Urusi ilishughulikiwa kwa sababu haikujibu tahadhari zetu,” rais wa Uturuki, Recep Erdogan alisema jana.

“IS hawako katika eneo la mpaka, lakini wanajeshi wa Uturuki walikuwa pale. Yeyote anaeshambulia eneo hilo anawashambulia kaka na dada zetu,” aliongeza rais Erdogan.

Kwa upande wa rais wa Urusi Vladimir putin alisema kuwa tukio hilo lina madhara makubwa kwa uhusiano wa nchi yake na Uturuki. Aliongeza kuwa tukio hilo linawakilisha kuchomwa kisu cha mgogoni na watu wanaowasaidia magaidi.

“Kuangushwa kwa ndege kunawakilisha kuchomwa kisu mgogoni na watu ambao wanawasaidia magaidi. Siwezi kuelezea kilichotokea katika njia nyingine,” alisema Putin na kuongeza kuwa ndege ya Urusi haikuwa inahatarisha amani ya Uturuki kwa namna yoyote.

 

Mtola Wa Simba Atimkia Geita Kwa Magufuli
Rais Kenyatta Awapiga Chini Mawaziri Wote Wenye Kashfa Za Ufisadi