Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (DRC), imemfukuza rasmi Balozi wa Rwanda nchini humo, Vincent Karega kwa kumpa saa 48 za kuwa tayari ameondoka jijini Kinshasa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Msemaji wa serikali ya DRC, Patrick Muyaya, imesema kutokana na nchi ya Rwanda kuendelea kuliunga mkono kundi la M23, baraza la ulinzi linaloongozwa na Rais, Felix Tshisekedi limemtaka Balozi huyo wa Rwanda kurudi nyumbani.

Waasi wa M23 waliopo Mashariki mwa DRC. Paicha: AllAfrica.com

Hatua hiyo, inakuja kufuatia kundi la waasi la M23 ambalo Congo inadai kuwa linaungwa mkono na Serikali ya Kigali, inayoongozwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame, likiendelea kupata nguvu katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Hata hivyo, inaarifiwa kuwa uamuzi wa kumtimua balozi wa Rwanda umefikiwa baada ya serikali ya Congo, kufanya tathmini juu ya hali ya usalama nchini humo na kuona ipo haja ya kuvunja balozi hiyo kama hatua mojawapo ya kutafuta salama ya eneo hilo.

Waitaka Serikali kutonyamaza kero za biashara
Rais athibitisha tukio la vifo watu 100