Rais wa Sri Lanka Gotabaya Rajapaksa amewafuta kazi ndugu zake wawili na mpwa wake kutoka kwenye baraza la mawaziri, hiyo ikiwa ishara wazi kwamba amekiri usimamizi mbaya wa mzozo wa uchumi nchini humo.

Wabunge kadhaa wa chama tawala cha Rais Rajapaksa wameigeuka serikali yake na vyama vya upinzani vimekataa mwaliko wa kujiunga katika serikali ya muungano.

Maandamano makubwa ya kuupinga uongozi wa Rajapaksa yamefanyika nje ya ofisi yake iliyoko pembezoni mwa bahari huku waandamanaji wakikita kambi kwa zaidi ya wiki moja, ambapo kiongozi huyo amekataa amekataa shinikizo la kumtaka ajiuzulu.

Serikali ya Sri Lanka inajiandaa kufanya mazungumzo na Shirika la Fedha Duniani IMF kwa ajili ya kunusuriwa kutoka kwenye mzozo huo wa kiuchumi.

Waziri Mkuu aipongeza TBC
Tshabalala afunguka watakavyoikabili Orlando Afrika Kusini