Rais John Magufuli leo amewaapisha jumla ya mawaziri na manaibu waziri 30 aliowateua.

Tukio hilo la kihistoria linaloashiria kuanza kazi rasmi kwa timu nzima ya serikali ya awamu ya tano limefanyika muda mfupi uliopita katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, bado masikio na macho ya watanzania yanasubiri kusikia majina ya mawaziri wanne waliosalia ambao rais Magufuli aliahidi kuwatangaza baadae kwa kuwa bado hajawapata.

Hii ni timu ya serikali ya awamu ya tano ¬†inayotarajiwa kufanya kazi kubwa usiku na mchana ili kutimiza ahadi za rais na kuendana na kauli mbiu ya ‘Hapa Kazi Tu”.

Mwakyembe Aomba Apewe Muda, azungumzia Katiba Mpya
Meneja CRDB ashikiliwa kwa Ujambazi, Ugaidi