Rais mteule wa wa Nigeria Bola Tinubu ametoa wito kwa wapinzani wake kuungana naye kwa ajili ya ujenzi wa taifa, baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa urais uliompa ushindi.
Ametoa kauli hiyo, wakati huu wagombea wakuu wa upinzani wakiendelea kukataa kutambua ushindi wake, huku Peter Obi aliyeibuka katika nafasi ya tatu, huku chama chake cha Labour kikisema kitakwenda Mahakama, kupinga ushindi wa Tinubu, wakati kikitoa wito wa utulivu kwa wafuasi wake.
“Kwa wale ambao hawakuniunga mkono, msikubali masikitiko hayo yawanyime fursa ya sisi kufanya kazi pamoja, ni lazima tuungane pamoja ilikupeleka nchi yetu mbele, naweza kuwa rais lakini nawahitaji zaidi, na raia wa Nigeria wanawahaitajhi hata zaidi.”amesema Tinubu
Wakati akipokea cheti chake cha rais mteule wa Nigeria, ameahidi kufanya kazi usiku na mchana kwa manufa ya raia wote wa Nigeria pamoja na kuifanya nchi hiyo kuwa bora tena.
Muhammadu Buhari rais anayemaliza muda wake, amemtaja mrithi wake Bola Tinubu kama mtu anayestahili kuliongoza taifa hilo baada yake kuondoka, Buhari akieleza kuwa ana imani na Tinubu.