Rais Mteule, Dkt. John Magufuli amedhihirisha msimamo wake wa kutaka kuwashughulikia baadhi ya wanachama wa CCM waliokuwa wakifanya kazi ya kukisaliti chama hicho wakati wa kampeni.

Akiongea baada ya kukabidhiwa Tuzo ya Ushindi na mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva, Dkt. Magufuli aliwataka wale wote waliokuwa wanakisaliti chama hicho na kuwasaidia viongozi wa Ukawa ili hali wakiwa ndani ya chama hicho (wasaliti) kujisalimisha mapema kwani mwisho wao umefika.

Alisema kuwa atabaki kuwa mkweli na hatawavumilia wasaliti hao ambao walifanya kazi ya CCM kuwa ngumu wakati wa harakati za kampeni.

Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake alipokuwa katika kampeni kwani aliwahi kuwasihili wale wanaofanya kazi ya CCM mchana na kisha usiku kuwasaidia Ukawa, kuacha mara moja vinginevyo aliahidi kuwashughulikia mara baada ya kushinda urais.

Dkt. Magufuli hakuficha na alikuwa akiwataja majina baadhi yao huku baadhi wakijitokeza na kujisafisha.

Katika hatua nyingine, Dkt. Magufuli aliwashukuru wote waliomuunga mkono na kusababisha ushindi wake kuwa mkubwa na aliahidi kufanya kazi kwa nguvu zake zote kuwatumikia watanzania kwa kipindi chote cha miaka mitano ya serikali yake.

 

 

Baada Ya Kushinda Udiwani, Baba Levo Kutumia Milioni 110 kufanya hiki Kigoma
Viongozi Wa Ukawa Waibukia Uholanzi..