Baba Levo ambaye hivi sasa ni mheshimiwa Diwani Mteule wa Kata ya Mwanga, Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT –Wazalendo, amepanga kubadili mazingira ya muziki Kigoma na kuwavuta wasanii wa Dar es Salaam katika mji huo kupitia uwekezaji wa zaidi ya milioni 110.

Msanii huyo wa Bongo Flava ameeleza kuwa baada ya kushinda udiwani, amepanga kutekeleza ahadi yake ya kuanzisha studio kubwa ya muziki zaidi ya studio zote zilizopo Dar es Salaam, uwekezaji utakaomgharimu kiasi hicho cha fedha.

“Inafunguliwa studio ambayo ni kubwa nadhani kushinda hata studio zote za Dar es Salaam lakini inafunguliwa Kigoma. Studio hiyo gharama yake ni kama milioni 110 hivi,” ameiambia The Chart ya 100.5 Times Fm.

Amesema kuwa lengo la kufungua studio hiyo ni utekelezaji wa sera za chama chake na wazo lake katika kukuza vipaji vya sanaa ya muziki na uigizaji na kwamba anataka wasanii kutoka nje ya nchi pamoja na Dar es Salaam wawe wanafunga safari kuelekea Kigoma Mjini kurekodi nyimbo zao.

Akizungumzia ushindi wa Udiwani alioupata, Baba Levo ameeleza kuwa ushindi huo kwake ni muhimu sana kwani alichagua kata iliyokuwa na ushindani mkubwa iliyokuwa mikononi mwa CCM kwa miaka 14.

Wizkid: R. Kelly Aliomba Kunishirikisha Kwenye Wimbo Wake
Rais Mteule Awatetemesha Walioivuta Shati CCM Wakiwa Ndani