‘Ojuelegba’ hitmaker, Wizkid ambaye leo yuko Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya show na ‘Live Band’, ameeleza jinsi alivyoweza kumkuna R. Kelly aliyefanya uamuzi wa kuwasilisha ombi lake kwake akitaka amshirikishe.

Akiongea na East Africa Radio leo, Wizkid ameeleza kuwa baada ya wimbo wake wa Ojuelegba kuwafurahisha mastaa wengi wa Marekani na kufanyiwa remix na Drake, alipokea simu kutoka kwa R. Kelly, simu iliyozaa collabo itakayokuwa kwenye album mpya ya Mfalme huyo wa R& B.

“I just did a record with R. Kelly… it is a record for his album,” alisema Wizkid.

Sio R. Kelly pekee aliyekiona kipaji cha Wizkid, wasanii wengine waliowahi kuonesha kumpigia salute ni pamoja na Alicia Keys pamoja na Rihanna aliyedai kuwa alimuita ‘amazing’.

Wizkid alishafanya collabo na Chris Brown, collabo ambayo inapatikana kwenye albam yake itakayotoka 2015.

Tailor Swift Atuhumiwa Kwa Wizi, Sheria Yamaliza Mzozo
Baada Ya Kushinda Udiwani, Baba Levo Kutumia Milioni 110 kufanya hiki Kigoma