Vyombo vya habari nchini Russia na Uingereza vimeripoti kuwa Rais wa Russia Vladimir Putin amepata watoto mapacha na mchumbawake wa muda mrefu.

Magazeti maarufu ya The Daily Telegraph na Daily Mail yamechapisha taarifa kwamba Putin mwenye umri wa miaka 66 na mchumbawake wa muda mrefu, mwanamichezo mstaafu, Alina kabaeva (36), wamepata watoto mapacha.

Kwa mujibu wa magazeti hayo Alina Kabaeva alijifungua katika hospitali moja ya kifahari na yenye ulinzi mkali ambayo ipo jijini Moscow.

Taarifa hizo zinadai kuwa mwanamichezo huyo wa zamani ambaye ni mshindi wa medali ya Olimpiki, ameamua kufanya siri ujio wa watoto wake na bado hajasema neno lolote.

Imeeleza kuwa suala hilo limewekwa siri na watu wa karibu wa mrembo Kabaeva wamekataa pia kuweka wazi kwenye vyombo vya habari, hata wale ambao walikuwa awali wanatoa ushirikiano kwa vyombo vya habari vya Moscow.

Hata hivyo, Sergie Kanev, mwandishi wa habari za uchunguzi anayefanya kazi kwa karibu na vyombo vya usalama vya Russia, amenukuliwa akisema mchumba wa Rais Putin amejifungua watoto mapacha kwa njia ya upasuaji.

Cardi B amehairisha tamasha kisa upasuaji
Trump, Spika watofautiana, asusia kikao

Comments

comments