Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara kwa sasa imesimama kwa takribani majuma mawili. Sababu kubwa ya kusimama kwa ligi hiyo ni kupisha Kombe la Chalenji la CECAFA – michuano inayoratibiwa na Baraza la Soka kwa nchi za Afrika Mashariki (CECAFA).

Michuano ya CECAFA itafikia ukomo Desemba 17, mwaka huu na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetoa ratiba mara baada ya michuano hiyo.

Desemba 22, 23, 24 na 26, zitakuwa siku za mechi za kuwania Kombe la Shirikisho la Azam yaani Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Mechi zitakazochezwa katika siku hizo zitafahamika Desemba 5, mwaka huu ambako imepangwa droo ya timu 64 zitakazocheza Raundi ya Tatu ya ASFC.

Timu 64 maana yake ni kuwa timu 16 za Ligi Kuu ya Tanzania Bara; timu 24 za Ligi Daraja la Kwanza na timu 24 ambazo zimefuzu kutoka hatua awali; ya kwanza na pili.

Baada ya michezo hiyo, ratiba ya Ligi Kuu itaendelea tena kwa michezo ya raundi ya 12 itakayofanyika Desemba 29, 30 na 31 kabla ya ligi tena kusimama kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Watanzania hawa kazini CECAFA
Magufuli afanya uteuzi mwingine