Mabondia waliowahi kutamba duniani wameendelea kuonyesha kuguswa na msiba wa bondia Mohamed Ali aliyefikwa na umauti akiwa na umri wa miaka 74.

Mabondia Sugar Ray Leonard, Mike Tyson wametoa heshima zao za mwisho kwa marehemu Ali: “Maombi na baraka kwa shujaa wangu, rafiki yangu na bila shaka bingwa wa wakati wote@MuhammadAli!”

Mara ya mwisho Ali kuonekana hadharani ilikuwa Aprili katika tamasha la “Celebrity Fight Night” mjini Arizona.

Ali aligundulika kuwa na ugonjwa wa Parkinson miaka mitatu baada ya kustaafu ndondi mwaka 1981 akiwa na rekodi ya kushinda mapambano 56 na kushindwa matano.

Sugar Ray Leonard na Mike Tyson

Ali aliingia kwenye mgogoro na serikali ya Marekani kwa zaidi ya miaka mitatu miaka ya 1960 wakati alipokataa kujiunga na jeshi la nchi hiyo kwa ajili ya vita ya Vietnam na akashitakiwa na kutiwa hatiani.

Mahakama ya juu kabisa ya Marekani ikaipundua hukumu hiyo na kauchiwa kabla ya kwenda kushinda mataji mawili ya dunia ya uzito wa juu kisha kustaafu mwaka 1981. Pumzika kwa amani fundi Ali. Dunia itakukumbuka daima.

Mbwana Samatta Awapa Nafasi Young Africans Dhidi Ya TP Mazembe
Allah Jaalia Ushindi Kwa Taifa Stars