Wababe wa Mji wa Madrid ‘Real Madrid’ wapo kwenye nafasi nzuri ya kumsajili Mshambuliaji wa PSG ya Ufaransa Kylian Mbape baada kumuajiri Mkurugenzi wa michezo wa zamani wa AS Monaco, Luis Campos.

Campos ambaye klabu yake ya mwisho kuitumikia kabla ya kujiunga na Real Madrid ilikuwa ni Lille ya Ufaransa, inadaiwa amekuwa na mahusiano mazuri na Mbappe, jambo linaloipa Real Madrid matumaini makubwa ya kumnasa mshambuliaji huyo katika kipindi hiki cha dirisha kubwa la usajili.

Campos ndiye anatajwa kutoa mchango mkubwa katika mafanikio ya Mbappe, kufuatia ushawishi usajili wa mshambuliaji huyo kwenye kikosi cha wakubwa cha AS Monaco wakati huo akichezea katika timu ya vijana.

Real Madrid inaamini ipo kwenye nafasi nzuri ya kumnasa nyota huyo, huku Mbappe akionesha nia ya kutoongeza mkataba mpya katika kikosi cha PSG.

Milioni 400 ujenzi daraja la Malagarasi
Simba SC yasajili beki 'KIMYA KIMYA'