Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani kagera, Agustino Olomi amesema kuwa chanzo cha wanafunzi kupoteza maisha na kujeruhiwa kwa bomu ni kutokana na Mwanafunzi kuokota bomu hilo akidhani chuma chakavu ili aweze kwenda kuuza.
Katika taarifa aliyoitoa wakati akizungumza na Wanahabari Kamanda Olomi amesema kuwa katika kijiji hicho kumekuwa na tabia ya kuuza vyuma chakavu ambapo mnunuzi huwa akiwapatia malipo ya madaftari.
Hata hivyo, Kwa upande wa Kamanda wa Kikosi cha kulinda mipaka cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Wilaya ya Ngara Meja Jenerali, TR Mutaguzwa amesema Bomu hilo lilikuwa na vipande 36 na lingelipukia ndani ya darasa lingeleta athari kubwa zaidi.