Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amempongeza Rais wa Kenya, William Ruto na kumtaka kutanguliza Ushirikiano wa soko la Afrika Mashariki ili kuleta maendeleo katika jamii. 

Museven, ameyasema hayo wakati wa uapisho wa Ruto na kusema alikuwa akifuatilia vyombo vya Habari vya ndani wakati wa uchaguzi, lakini ushirikiano wa Afrika Mashariki haukushughulikiwa vyema.

 “Nilichopata tatizo walikuwa hawaongelei ushirikiano wa Afrika Mashariki, bali Kenya pekee, Ili nchi za Afrika Mashariki zifikie Marekani, zinapaswa kuangalia soko la kanda,” amesema Museveni.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Kenya, William Ruto.

Kwa upande wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameipongeza Kenya kwa kudumisha amani katika kipindi cha uchaguzi na kudhihirisha kuwa kukabidhiana madaraka kwa amani kunawezekana. 

Naye, Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye amewapongeza wananchi wa Kenya kwa kufanya uchaguzi wa amani na kusema, “Kenya imeshinda na mafanikio yako ni fahari ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Umemshinda shetani wa jeuri. Hongera sana.”

Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki wamehudhuria hafla ya kuapishwa kwa mwanachama mpya wa Jumuiya hiyo, Rais wa Jamhuri ya Kenya William Ruto uliofanyaika leo katika uwanja wa michezo wa Kasarani semptemba 13, 2022.

Kinda la Tanzania limeanza maisha mapya Barcelona
Juma Mgunda achimba mkwara mzito Simba SC