Wakili wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake watatu amesema hawakuridhika na uamuzi wa mahakama hivyo wanatarajia kukata rufaa.

Akizungumza jana na waandishi wa habari muda mfupi baada ya wateja wake kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja kwa kukutwa na hatia ya unyang’anyi wa kutumia silaha, Wakili huyo amesema hukumu iliyotolewa ina mapungufu mengi.

Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Odira Amworo alitoa hukumu hiyo dhidi ya Sabaya na wenzake alieleza kuwa baada ya kupitia ushahidi uliwaosilishwa na upande wa mashtaka pamoja na vielelezo, Mahakama hiyo imejiridhisha kuwa walienda kwenye duka la shahidi wa kwanza wakiwa na silaha.

Hivyo, Hakimu alieleza kuwa kulikuwa na ushahidi kuwa duka hilo lilivamiwa na watu wenye silaha na lilikuwa chini ya watu wenye silaha.

Simulizi: Wanetu kukosa akili darasani kulivyohatarisha Ndoa yangu
Profesa Mchome awafunda Mawakili wasomi