Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, amejibu madai ya kuomba rushwa ya Mil. 5 yaliyotolewa na mmoja wa wafanyabiashara wa Hoteli za Kitalii mkoani Kilimanjaro, katika mkutano wa wadau wa Utalii mkoani humo, ambapo Sabaya amedai suala hilo limeanzia kwenye mgogoro wa ardhi.

Ameyasema wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wakati akizungumza na wananchi, ambapo amesema kuwa amekuwa akipokea simu mbalimbali zikimtaka ajibu tuhuma hizo, juu ya matumizi mabaya ya ofisi yake.

“Chanzo cha yote hayo ni Bibi aliyelalamika kwangu kuhusu shamba lake kuvamiwa, niliunda Kamati Maalum ambayo iliyoongozwa na Katibu Tawala, Afisa ardhi na Mwanasheria, waliponiletea taarifa ilionyesha bibi huyo analimiliki tangu 1971, OCD nakuelekeza kwa sababu yeye ametoa tuhuma zake akijua leo nakuja kufanya maamuzi, kwanza OCD muhakikishie huyo mfanyanyabiashara Cathibert Swai usalama wake na umtake ajibu mashtaka ya kudhulumu haki za hawa watu,” amesema Sabaya.

Aidha, siku za hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii, kulisambaa kipande cha video kikimuonyesha moja ya wafanyabiashara wa Hoteli za Kitalii mkoani Kilimanjaro, aliyefahamika kwa jina la Cathebert Swai akimlalamikia Ole Sabaya kwa matumizi mabaya ya ofisi yake.

Hata hivyo, malalamiko ya mfanyabiashara huyo alisema kuwa DC Sabaya alimpa masaa 48 kuhamisha akaunti zake za benki kwenda Hai bila sababu yeyote ya msingi., wakati huo huo akawa anadai fedha ambayo hatakiwi kulipa kwa mujibu wa sheria na alifika ofisi kwa mfanyabiashara huyo na kupewa kiasi cha shilingi milioni 5.

“Achana na hiyo mwaka jana mwezi wa 11, alinipa masaa 48 kuhamisha akaunti zangu za benki kwenda Hai bila sababu yeyote, wakati huohuo akawa ananidai fedha ambayo sitakiwi kulipa kwa mujibu wa sheria, na kuna siku alikuja ofisini kwangu akinitaka nimpe milioni 5, nikawa sina budi ikanibidi nimpe tu tena kwa mafungu mafungu,”amesema Swai

Rais Magufuli achangia Sh 400 milioni kujenga kituo cha afya kijijini
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 26, 2019