Ujio wa album mpya ya Rihanna iliyopewa jina la ‘Anti’ unaonekana kuwa na neema ya aina yake ambapo inaripotiwa kuwa album hiyo imepata ufadhili mnono kutoka kampuni ya Samsung.

Kwa mujibu wa New York Post, Samsung na Rihanna wanashirikiana kwa udhamini wa $25 million, kiasi ambacho ni mabilioni ya shilingi ya Tanzania.

Kiasi hicho kinadaiwa kuwa kiwango kitakachofadhili albam yake ya nane ‘Anti’ pamoja na ziara kubwa ya kuizunguka dunia.

Samsung wamepanga kuutumia muziki na video za Rihanna kutangaza huduma zao za ‘streaming’ pamoja na simu zao mpya.

Hii si mara ya kwanza kwa Sumsung kufanya udhamini kama huu, mwaka 2013, walidhamini album ya Jay Z ‘Magna Carta.. Holy Grail’, kwa $5 million, ambapo wateja wa Samsung Galaxy milioni 1 waliweza kuipata album hiyo siku tatu kabla ya siku ya kuitoa rasmi.

Ruby: Niliandaliwa Kucheza Mpira Wa Miguu Ngazi ya Taifa
Rapper Wa Marekani Aliyejiunga Na ISIS Auwawa, Ni Rafiki Wa DMX