Naibu Waziri wa Mifugo na Uvivu, Abdallah Ulega, amesema Serikali inatarajia kuwakopesha Wavuvi nchini kote Boti za kisasa zaidi ya 150, zitakazowawezesha kuboresha shughuli zao za uvuvi.

Ulega, ameyabainisha hayo wakati wa ziara yake ya Kanda ya ziwa, na kusema ili wavuvi waweze kuongeza uzalishaji wa samaki.

Umati wa Wananchi waliokuwa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvivu, Abdallah Ulega.

Amesema, boti hizo zitafungamanishwa na teknolojia za kisasa zitakazomsaidia mvuvi kurahisisha shughuli za uvuvi na kufanya biashara zao kuwa za kisasa zaidi na kuongeza wigo wa soko.

Waziri Ulega amefafanua kuwa, Rais Samia anataka kuwatoa Wavuvi katika uvuvi wa kuwinda na kufanya ufugaji wa kisasa wa Samaki utakaowapatia uhakika wa biashara zao.

Wanywaji Pombe za kienyeji waing'ata sikio Serikali
TAWA yatumia 'Marathon' kutangaza Utalii