Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi Na Mawasiliano kwa kushirikiana na kampuni ya Oracle wameandaa mkutano wa wataalamu wa Tehama kutoka nchi mbalimbali duniani,mkutano huo utafanyika kesho jijini Dar es salaam.

Wizara ya ujenzi kwa kupitia kaimu mkurugenzi wa idara ya Tehama wa wizara hiyo Dkt.Shaban Pazi alisema,Tanzania inakua mwenyeji wa mkutano huo sababu kubwa ikiwa ni pamoja na kupiga hatua kubwa  ya kiteknolojia kwa muda mfupi zaidi hivyo kumeifanya kampuni hiyo ya Oracle inayojishughulisha na mitandao kuamua kuja Tanzania.

Aidha Dkt,Pazi alibainisha kwamba lengo kubwa la mkutano huo ni  usalama wa data na Usalama wa taarifa mbalimbali za Serikali na kuhakikisha hakuna tena upotevu wa data na fedha kupitia mitandao inayofanywa na wahalifu.

Vilevile Dkt Pazi ameelezea mafanikio ambayo Serikali imeyapata kwa kukamilisha Ujenzi wa wa mkongo wa taifa na,kujenga kituo  cha kuhifadhi data na kuaandaa Sheria za mitandao ambazo zitasaidia kupunguza matumizi mabaya ya mitandao.

Video: Shirika la kazi Duniani kuandaa tuzo kwa Waajiri
Video: Baada ya Mahakama kutengua matokeo ya Mbunge Nangole (Chadema), Dk. Kiruswa (CCM) amesema.....