Leo Juni 1, 2018 Serikali kupitia Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, na Walemavu, Anthony Mavunde imesema inaandaa utaratibu maalumu wa kutoa ajira za moja kwa moja kwa wanafunzi wa fani mbalimbali za ufundi kutoka vyuoni ili kuepusha usumbufu wanaopata katika kutafuta ajira mara baada ya kuhitimu masomo yao.
“Tunachokifanya kama Serikali kwanza kabisa kwa kushirikiana na Sekta binafsi ambapo pindi nafasi zinapopatikana huwa tunaunganisha moja kwa moja na vyuo vyetu vya ufundi ili vijana hawa waweze kupata nafasi za ajira za moja kwa moja, sisi kama Serikali tutaona namna ya kuunganisha vyuo vyetu vya ufundi pamoja na waajiri nao wapate nafasi za moja kwa moja” amesema Mavunde
Mavunde ameongeza kuwa serikali itatumia mfano wa baadhi ya vyuo vya ufundi kikiwemo chuo cha Don Bosco ambacho hufanya kongamano wadau wa fani za ufundi ili kuweza kutoa fursa za ajira kwa vijana wanohitimu katika chuo hicho.
-
Tanzia: Mama mzazi wa Mbunge Bashe ameaga dunia mapema leo
-
Kujipima ukimwi nyumbani kwazua sura mpya
Kwa upande mwingine Mavunde huyo amedai kuwa Serikali imeweka vituo vya kulea vijana ambavyo ni Sasanda (Mbeya), Ilonga (Morogoro) na Kilimanjaro lengo likiwa ni kuandaa vijana kuwa na sifa za kuajirika na pia Serikali imetenga mfuko wa maendeleo ya vijana ili kutoa mikopo kwa vijana.