Serikali nchini, kupitia Wizara ya Nishati imesema imekamilisha mashauriano na wawekezaji wa mradi wake wa gesi asilia ya mmiminiko (LNG) wenye thamani ya dola bilioni 42, na mikataba iko tayari kuangaliwa ili kuidhinishwa mwezi ujao.
Waziri wa Nishati, January Makamba ameyasema hayo na kuongeza kuiwa uidhinishwaji wa mikataba ya mradi huo ambao umechelewa kwa muda mrefu- inalenga uchimbaji wa rasilimali kubwa ya gesi iliyoko nchini lakini asilimali iko baharini na mikataba hiyo itawasilishwa katika baraza la mawaziri kabla ya kusainiwa.
Aidha, Makamba katika wasilisho lake hakutoa muda maalum katika maelezo yake bungeni, hotuba ya bajeti ya wizara ya nishati kwa mwaka 2023/24 iliyochapishwa katika tovuti yake ilionyesha kuwa mwezi Juni wawekezaji wa LNG na serikali wanatarajiwa kusaini makubaliano ya ushirikiano wa uzalishaji uliofanyiwa marekebisho.
Alisema, “Mradi huo wa dola bilioni 42 utabadilisha taswira na sura ya uchumi wetu,” alisema Makamba huku ikikumbukwa kuwa makampuni ya Equinor, Shell na Exxon Mobil walisema wamefikia makubaliano na nchi hiyo ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kuendeleza kituo cha mauzo ya nje cha LNG.