Wakala wa Mbegu za kilimo Tanzania – ASA, imesema katika msimu huu wa kilimo wa mwaka 2023 inatarajia kuongeza uzalishaji wa mbegu za mazao ya kilimo kutoka tani 3300 za awali na kufikia tani zaidi ya 6000 kutokana na serikali kuongeza uwekezaji katika mashamba ya uzalishaji mbegu.

Mkurugenzi uzalishaji wakala wa Mbegu za kilimo Tanzania ASA Justin Lingo amesema taasisi hiyo ni moja ya taasisi pekee iliyopewa ithibati ya kuzalisha mbegu bora za mazao ya kilimo hapa nchini ili kumuwezesha mkulima kuweza kutumia mbegu bora ambazo zinaweza kutoa mazao bora na yenye uwezo wa kushindana katika soko la ndani na nje ya nchi.

Kutokana na serikali kuongeza uwekezaji katika mashamba ya kuzalisha mbegu, mpango uliopo kwa sasa ni kuongeza uzalishaji wa mbegu za mazao mbalimbali ya kilimo, Lingo anasema kwa sasa upo mkakati maalumu wa kuwafanya vijana nchini kukipenda kilimo kwa kuwafundisha angali wakiwa na umri mdogo ambao utasaidia kukuza sekta ya kilimo.

Katika kuhakikisha vijana wanapenda kilimo, Kituo cha kulelea watoto yatima cha Mgolole kilichopo manispaa ya Morogoro wanafanya ziara ya kutembelea mashamba ya uzalishaji wa mbegu kwa lengo la kujifunza.

Baracka Daniel ni Mkuu wa kitengo cha Uhaulishaji wa Teknolojia na mahusiano kutoka TARI anasema kwa sasa upo mkakati maalum wa kushirikiana na taaissi zote zinazohusu kilimo ili kuongeza tija ya uzalishaji wa zao hilo

Nao watoto wa kituo hicho wameishukuru Taasisi ya uzalishaji begu ASA kwa elimu hiyo na kwamba wanaamini itakua yenye tija kwao.

Kamati ya maridhiano CCM, ACT yazinduliwa Zanzibar
Wanaouzaji ardhi kiholela waonywa, waelimishwa