Naibu Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye ametoa onyo kwa wazazi na walezi wanao waruhusu watoto walio chini ya umri wa miaka 18 kumiliki simu na laini za mawasiliano kwani ni kinyume na sheria ya mawasiliano.

” Sisi kama Serikali tunasema mtu ambaye hajatimiza miaka 18 haruhusiwi kumiliki simu maana hawezi kusajiliwa kumiliki laini, unakuta namba ya simu imesajiliwa na mtu mwingine ili mtoto aitumie, sasa huyo mwingine sisi ndiye tutakaye mkamata” amesema Mhandisi Nditiye

Ameongeza kuwa endapo simu ikasajiliwa na akapewa mtoto atumie, ikamletea madhara, serikali itaiweka kwenye mfumo wa kuangalia na aliyesajiliwa ndiye atakuwa shahidi namba moja kulingana na madhara atakayokuwa ameyapata mtoto.

Aidha Mhandisi Nditiye amesema kuwa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole hadi sasa umefanikiwa kwa asilimia zaidi ya 70, hivyo zoezi linaenda vizuri, na ameongeza kuwa lengo kuu la Serikali ni kuhakikisha wananchi wanafurahia huduma ya mawasiliano bila tatizo.

 

 

 

 

Stars yaanza maandalizi kuichakaza Burundi Kuelekea kombe la Dunia
Hakimu atoa nafasi ya mwisho kesi ya Mdee