Serikali nchini, imekiri kuridhishwa na kasi ya Ujenzi wa mradi wa Bwawa la kuzalisha umeme Rufiji Mkoani Pwani, ambapo umefikia asilimia 85.06
Hayo yamebainishwa hii leo Aprili 25, 2023 na Waziri wa Nishati, Januari Makamba ambaye amesema mwenendo wa kujaza maji ni wa kuridhisha kutokana na lita za ujazo Bilioni sita kuingia kwenye Bwawa hilo.
Amesema, “kazi zinazoendeela hivi sasa ni pamoja kuunganisha vipuri kwenye kitambo itakayotumika kufua Nishati ya umeme mradi huu ji mkubwa na umeme wa Mtera wa Megawati 80 hapa ni mashine moja pekee, niwapongeze TANESCO kwa jitihada.”
Aidha, Makamba ameongeza kuwa Bwawa hilo litawezeaha kupatikana kwa megawati 2115 za Nishati ya umeme ambazo zitasaidia kusongesha mbele gurudumu la maendeleo kwa kuwa na umeme wa uhakika.
Hata hivyo, kiwango cha maji kinachohitajika ili mitambo ya JNHPP ianze kufua umeme ni lita za ujazo ;ilioni 30 na hadi sasa zimeshapatikana lita Bilioni sita kwa msimu mmoja pekee wa mvua.
Kwa upande wake, Mhadishi Mkazi wa Mradi huo, Lutengano Mwandambo amesema maeneo ambayo yameshakamilisha yanafanya uwepo wa asilimia 15 pekee zilizobaki ili ukamilishwaji wa mitambo ya kuzalisha umeme ianze kufanya kazi.