Licha ya kupigwa vita na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, imebainika kwamba shisha ni chanzo cha mapato ya Serikali.

Utafiti uliofanywa na MTANZANIA na kuthibitishwa na baadhi ya wabunge, shisha inatambuliwa na sheria ya kodi ya mwaka 2016 iliyopitishwa na Bunge Juni mwaka huu kama chanzo cha mapato.

Ushuru wa “cigar” pamoja na sigara nyingine za kutoka nje, zilielezwa kuwa  uchumi unabaki kuwa asilimia 30 huku tumbaku ambayo iko tayari kutengeneza sigara (cut filler) ikipanda kutoka shilingi 24,388 hadi shilingi 25,608 kwa kilo.

Katika bajeti kuu ya Serikali iliyosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango Juni mwaka huu shisha ni mojawapo ya vyanzo hivyo ikiwa katika kundi la mazao yatokanayo na tumbaku.

Aidha baadhi ya wabunge wa Kamati ya Bunge ya Bajeti waliiambia MTANZANIA kuwa kilevi hicho (shisha) ni miongoni mwa vyanzo halisi vya mapato ya Serikali na kwamba kuipiga marufuku ni kukataa mapato halali ambayo yamewekwa kisheria.

Mbunge wa Momba, David Silinde (Chadema) alisema katazo lolote kuhusu bidhaa hiyo ya shisha ni batili kisheria.

Video Mpya: Vanessa Mdee: Cash Madame
Azam FC Yaanza Kujiwinda Azam Complex