Wamiliki wa shule binafsi nchini wametakiwa kuwasilisha serikalini mapendekezo ya ongezeko la ada kwa ajili ya hatua zaidi.

Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Profesa Sifuni Mchome amefafanua kuwa serikali haijazuia kuongeza ada kwa shule hizo bali wamiliki wanapaswa kuwasilisha mapendekezo ya ongezeko la ada hizo ili kuepuka kuongeza ada kiholela.

“Kwa mara nyingine tena kupeleka taarifa zao kwa msajili wa shule ambaye ndiye msaidizi wa kamishna katika masuala kama haya. Hakuna kinachowazuia kuongeza hizo ada ama kuleta mapendekezo ya kuongeza ada kwa mwaka 2016. Lakini kufanya hivyo kimyakimya ni kinyume na taratibu,” alisema Profesa Mchome.

Aliongeza kuwa serikali itapitia mapendekezo hayo na kutoa muongozo ili ada itakayokuwa ikilipwa na wananchi iendane na huduma inayopatikana katika shule husika.

BAKWATA yamtungua mkurugenzi wake, Ni Sakata la Kadhia ya Magari 82 na misamaha ya kodi
Arsene Wenger Na Arsenal Yake Kujihukumu Leo