Klabu ya Simba ipo mbioni kuongeza nguvu kwenye safu yake ya ushambuliaji na mlinda mlango baada ya kocha mkuu wa timu hiyo Joseph Omog kuona mapungufu kwenye maeneo hayo.

Kwa mujibu  wa Katibu Mkuu wa klabu hiyo Patrick Kahemele, kocha Omog amedai kwamba safu anahitaji mshambuliaji wa kuweza kusaidiana na Danny Lyanga na Ibrahim Ajib huku kwa upande wa kipa akitajwa kutafutwa kipa mwenye uzoefu atakayesaidiana na mkongwe Vicent Angban na kuwapa uzoefu makinda Manyika JR na Denis Richard.

Kahemele ameongeza kwamba, tayari wameanza kufanya mazungumzo na klabu ya Azam kwa ajili ya kupata saini ya mshambuliaji wa timu hiyo Ame Ally ambaye anaonekana kuwa na nafasi finyu katika timu hiyo.

“Tumepokea mapendekezo ya kocha mkuu, Joseph Omog akitaka tuongeze nguvu maeneo kadhaa mfano anataka tusajili golikipa mwingine mwenye uzoefu ili ampe Changamoto Angban (Vicent) pamoja na wale vijana (Manyika JR na Denis Richard).

Pia anataka mshambuliaji, tunao washambuliaji wazuri kama Lyanga na Ajibu, lakini wote ni aina moja ya uchezaji, ametaka tutafute Mwingine, na hivi sasa tupo kwenye mazungumzo na Azam tukitaka kumsajili Ame Ally.

Bahati nzuri Azam wao wana washambuliaji, kuna wengine wanawatoa, tunaamini mambo yakienda sawa, Ame tutakuwa naye”. Amesema katibu mkuu wa Simba, Patrick Kahemele.

Tayari Azam FC wameshaongeza mshambuliaji mwingine, Bruce Kangwa, kwahiyo nafasi yake huenda ikiwa ndogo ikizingatiwa kocha mkuu Zeben Hernandez alishaonesha dalili za kutomkubali Ame.

Video: Pesa ninazozipata ni nyingi kuliko Ubunge - JB
Video: Msanii ajipiga risasi mdomoni na kupost video Facebook akitafuta ‘Kiki’