Kamati ya utendaji ya klabu ya Simba imemsimamisha nahodha wake msaidizi Hassan Isihaka kuichezea klabu ya Simba kwa muda usiojulikana.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya mchezaji huyo kumtolea maneno yasiyo na staha kocha wa Simba Jackson Mayanja kabla ya mechi ya Jana ya kombe la shirikisho dhidi ya Singida United.

Kutokana na kitendo hicho kisicho cha kiungwana kilichofanywa mbele ya wachezaji wenzake na kinachokiuka waraka wa maadili(code of conduct)

Kamati ya utendaji licha ya kumsimamisha mchezaji huyo pia imeagiza alipwe nusu mshahara katika kipindi chote cha adhabu yake!

Pia kamati hiyo imewataka wachezaji wote kuzingatia nidhamu na weledi katika kipindi chote wanapoitumikia klabu ya Simba.

Imetolewa na Haji S.Manara
Mkuu wa idara ya mawasiliano wa klabu ya Simba.

Waziri Mkuu amtumbua Jibu Daktari aliyedaiwa kupokea Rushwa na kukacha Uparesheni
Ajib Akabidhiwa Tuzo Ya Mchezaji Bora