Mkoa wa Songwe ni miongoni mwa mikoa iliyopo mipakani ambapo kumekuwa wimbi kubwa la wahamiaji haramu ambao wamekuwa wakiingia nchini kinyume cha sheria,

Katika jitihada za kuhakikisha tatizo hilo linamalizika, Jeshi la Polisi na Idara ya Uhamiaji limeamua kushirikiana na wananchi kuanzisha msako mkali ambao umefanikisha kuwakamata wahamiaji haramu 15 kutoka nchini Ethiopia.

Aidha, Wahamiaji hao walikamatwa wakiwa wamehifadhiwa katika shamba la mahindi lililopo katika Kijiji cha Ipumpila Wilaya ya Momba Mkoani Songwe wakiwa katika harakati za kusafiri kuelekea Afrika ya Kusini.
Hata hivyo, Afisa Uhamiaji Mkoa wa Songwe, Elizeus  Mshongi amesema  tukio hilo limetokea wakati ambapo tayari raia wengine watano wa Ethiopia wameshakamatwa na kahukumiwa kwenda jela.

Pia ameongeza kuwa changamoto kubwa iliyopo ni wahamiaji haramu hao kusaidiwa na Watanzania wanaojua njia za  maficho na kuongeza kuwa watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kukabiliana na mkono wa sheria.

Magazeti ya Tanzania leo Aprili 10, 2017
Ney wa Mitego Avutana na 'Askari' Kanzu Aliyekuwa Anamrekodi